Augustinian hypothesis
MUHUTASARI WA NADHARIA YA AUGUSTINO MTAKATIFU ( Augustinian hypothesis) Agostino alizaliwa tarehe 13 Novemba 354 katika mji wa Thagaste mkoa wa Numidia nchini Algeria. Ni miaka michache tu baada ya ukristo kupewa uhuru wake na dola ya Kirumi mnamo mwaka 313 chini ya utawala wa mfalme Konstantino. Jina lake aliitwa Aurelius Augustinus mara baada ya kuzaliwa . Baba yake aliitwa Patrisi anasadikika kutokua mkristo bali aliabudu miungu mingi, inasemekana amekubali na kubatizwa mwishoni mwa maisha yake. Na mama yake ni Monika , mpaka sasa anaheshimiwa kama mtakatifu alikua mkristo kweli aliyemuwezesha mwanae Konstatino kukulia maisha ya ukristo na kumlea kiimani. Tofauti na kulelewa katika maisha mazuri ya ukristo na mama yake bado Agustino wakati wa ujana wake aliishi maisha ya anasa na uzushi, baadae alifanikiwa kupata elimu katika lugha na uwezo wa kuhubiri huko Thagaste. Aliongoka mwaka 386 na kubatizwa mwaka 387 usiku wa kuamkia pasaka na askofu Ambrosi, hapo ukianga...