Augustinian hypothesis
MUHUTASARI WA NADHARIA YA
AUGUSTINO MTAKATIFU (Augustinian
hypothesis)
Agostino alizaliwa tarehe 13 Novemba
354 katika mji
wa Thagaste
mkoa wa Numidia
nchini Algeria. Ni miaka michache tu baada ya ukristo kupewa uhuru wake na dola
ya Kirumi mnamo mwaka 313 chini ya utawala wa mfalme Konstantino. Jina lake
aliitwa Aurelius Augustinus mara baada ya kuzaliwa. Baba yake aliitwa
Patrisi anasadikika kutokua mkristo bali aliabudu miungu mingi, inasemekana
amekubali na kubatizwa mwishoni mwa maisha yake. Na mama yake ni Monika,
mpaka sasa anaheshimiwa kama mtakatifu alikua mkristo kweli aliyemuwezesha
mwanae Konstatino kukulia maisha ya ukristo na kumlea kiimani.
Tofauti na kulelewa katika
maisha mazuri ya ukristo na mama yake bado Agustino wakati wa ujana wake
aliishi maisha ya anasa na uzushi, baadae alifanikiwa kupata elimu katika lugha
na uwezo wa kuhubiri huko Thagaste. Aliongoka mwaka 386 na kubatizwa mwaka 387
usiku wa kuamkia pasaka na askofu Ambrosi, hapo ukiangalia alikua na miaka 32.
Baada ya kubatizwa aliishi maisha ya kitawa na mnamo mwaka 391 akapewa daraja
la upadre katika mji wa Hippo alioutumikia mpaka mwaka 395, na miaka miwili
baadae (mwaka 397) akateuliwa kua askofu wa jimbo la Hippo. Baada yakuingia
rasmi katika kazi ya Mungu alijitoa kwa kila namna kuhakikisha anafundisha,
anaelekeza na kufafanua mafundisho sahihi ya ukristo ili kuwaelekeza wakristo
katika kumtumikia Mungu kwa usahihi (yaani alilenga kweli haswa) kuliko vitu
vingine. Aliandika maandiko mengi zaidi yenye mafundisho ya kiroho ndani yake
yanayofuatwa na watu wengi mpaka sasa.
Inasaidikika kati ya mababa wa
kanisa ndiye baba wa kanisa aliyeacha maandishi mengi zaidi, Maltin Luther
mwenyewe amekiri kua Augustino amekua baba wake wa kiroho pamoja na Paulo.
Baadhi ya maandiko yake ni
Ni miongoni mwa waandishi
walioandika nadharia mbalimbali ikiwepo nadharia ya matatizo ya kisinoptiki
katika agano jipya inayozihusisha injili za Mathayo, Marko na Luka, nadharia
hii ndiyo tutakayoiangalia kwa undani.
Nadharia ya Augustino
Hii ni nadharia inayojaribu
kutoa majibu ya injili ipi iliandikwa ya kwanza kati ya Mathayo, Marko na Luka,
ambapo alisema Mwinjilist Mathayo aliandika injili yake akiwa wa kwanza baadae
akafuatia Marko ambaye alitumia maandiko ya Mathayo na mafundisho ya Peter
(aliyesadikika kutembea nae pamoja katika ziara mbalimbali za kueneza injili ya
Kristo) kama chanzo. Pia alisema kua Mwinjilist Luka ndiye aliyeandika baadae
akizitumia injili za Mathayo na Luka katika uandishi wake kama inavyoelezwa
katika kitabu cha Luka 1:1-4. Tofauti ya nadharia hii na nyingine ni kwamba
Augustino amejikita zaidi katika ushaidi wa kihistoria kupitia maandiko
yaliyoandikwa na mababa wa kanisa mapema mwa karne ya pili ambayo bado yalikua
yakishikiliwa na wakristo bila kuangalia mfumo wa kiuandishi katika injili hizo
tatu.
Wafuasi wa maandiko ya nadharia
ya Augustino waliona kua nadharia yake ni nyepesi na yenye mawazo yakufikirika
zidi ya matatizo ya kisnoptiki. Nadharia hii ilizua maswali mengi kama vile ni
kwa namna gani mila za ukristo wa kwanza zitegemewe, injili ipi iliandikwa kwanza
sasa, je kuna chanzo kilichofichika nyuma?, haya na mengine yaliibuka ambayo
yalichochea uandishi wa nadharia nyingine ili kuleta ukweli wa injili ipi
iliandikwa kwanza, kama vile nadharia ya vyanzo viwili, uhusiano wa nadharia ya
chanzo-Q, nadharia ya Farrer na nyinginezo.
Maeneo mengine makuu mawili ya
ubishi kwenye jumuiya ya Augustino ni juu ya injili ya Mathayo kama mwanzo
iliandikwa katika lugha ya kiebrania au iliyoandikwa kwa Kiyunani ndio ya
mwanzo iliyoandikwa na mwinjilisti Mathayo. Pia kulikua na ubishi wa nani
ameandika akiwa wa kwanza kati ya Marko na Luka, nadharia ya Griesbach (Griesbach hypothesis) inasadikika kubadili
kidogo nadharia ya Augustino na kukubalia na kwamba Mathayo aliandika
akifuatiwa na Marko pia Luka ila haiongelei kama injili ya Mathayo ilikua ya
kiebrania kwanza au kiyunani hivyo ikahesabia kama marekebisho ya nadharia ya
Augustino.
Baadhi ya mababa wa kanisa
walioandika juu ya mpangilio wa injili kama Irenaeus,
Origen,
Eusebius
na wengine walikuabaliana na mawazo ya Augustino kua Mathayo aliandika wa
kwanza katika lugha ya kiebrania akifuatiwa na Marko pia Luka. Tuangalie
ushaidi wao kwa ufupi;
Papias:
Kulingana na maelezo ya Iranaeus, Papious ni miongoni mwa mashuhuda wa John pamoja
na Polycarp zamani hizo nae pia katika kitabu chake alisema kua Mwinjilisti
Mathayo aliandika injili akiwa wa kwanza. Aliandika kwamba “Mathayo alikusanya
maoni yake katika lugha ya kiebrania na kila mmoja akatafsiri katika lugha yake
awezavyo”.
Clement: Eusebius pia alinuukuu jumbe muhimu kutoka
kwa Clement wa Alexandria: alikua
akisema kua Injili za kwanza ni Mathayo na Luka ila injili ya Marko ilitokea
baada ya Marko kua na Peter katika kueneza injili huko Rumi, wakati huo aliweza
kusikiliza yote yaliyosemwa na Petero kama injili ya Yesu na kuaandika ili
yatumike kwa wote watakaohitaji kupata mafundisho hayo, Petero alipata taarifa
hizo na hakupinga au kutia mkazo sana.
Irenaeus: Irenaeus aliyekua akijua juu ya kazi ya
Papias na akimjua Polycarp na inasemekana alimjua pia mtume Yohana aliandika
akisema: “ Sasa Mathayo alichapisha kitabu chake cha inijili kwa lugha ya
kiebrania mwenyewe, wakati huo Petero na Paulo walikua wakihubiri injili Rumi
na kuanzisha kanisa. Yeye alitofautiana na wenzake kwa kusema kua injili ya
Marko iliandikwa baada ya kifo cha mtume Petro na wakati Papias na Clement
walisema Petro alikuwepo nakuiona kazi ya Marko. Lakini hii haikua hoja ya
kukataa nadharia ya Augustino maana yeye hakuongelea kuwepo au kutokuwepo kwa
Petro katika kipindi cha uandishi wa injili ya Marko.
Tunaweza
kuona na kutambua mchango mkubwa wa nadharia ya Augustino mtakatifu ilivyoweza
kufungua milango ya mahojiano zaidi ili kujua ni injili ipi iliandikwa kwanza
katika mpangilio wa injili tatu za kisnoptiki.
Comments
Post a Comment