Ijue zaidi biashara ya juice

Leo tunaendelea Na biashara ya juice changamoto na namna gani unavyoweza kuimudu

Changamoto zinazoweza kupatika katika biashara ya juisi

Kuharibika:

Kutokana Na kuwa juisi unayotengeneza haina kemikali yeyote iliyoongezwa ili kuitunza hivyo huweza kuharibika pindi ikikaa kwa mda wa zaidi ya saa 24.

Kumbuka Juisi atakayopeleka mteja aliyesambaziwa ataiweka kwenye jokofu lake Na kawaida ya wafanyabiashara hawezi kuwasha jokofu mda wote hivyo uhakika wa Juisi kukaa kwa mda mrefu unakuwa mdogo.

nini kifanyike

1. Usitengeneze Juisi nyingi wakati unaanza
tengeneza Juisi kidogo huku ukizidi kupanua masoko yako. Hii itakusaidia kuzijua changamoto zinazokupata zikiwa kidogo Na kuzitatua bila ya kupata hasara kubwa sana.

2. Weka Juisi kidogo kwa mfanyabiashara

wakati mnaanza biashara usizidi pakiti tano kwa sehemu inayochangamka Na pakiti tatu kwa duka linadolola.

3. Fungasha Juisi za bei ya chini

kuanzia miatatu Na miambili ikiwezekana Na za Mia Mia  usifungashe za miatano maana makampuni makubwa yanatengeneza Juisi za bei hiyo hivyo hutaweza ushindani utakuwa mkubwa.

4. Kila siku hakikisha Unafanya ukaguzi kwa wafanyabiashara uliowasambazia Juisi zako

ili kuangalia kama kuna Juisi zilizokaa zaidi Na zinaweza kuwa zimehatibika uzibadirishe. Kubali kuingia hasara hii maana itakufanya uimarishe soko lako Na kulilinda.

Kama hutabadirisha mfanyabiashara mwingine anaweza kuwapatia Juisi kama zilivyo Na kujikuta wateja wanahama kutumia juice zako. Sio hasara kwa mfanyabiashara kuona Juisi hazina wateja tena akaacha kuziuza tena Na wewe kupunguza soko. Biashara ikipanuka kazi hii unaweza kumpa mtu mwingine ili kupunguza majukumu Na kumudu usimamizi

5. Usipende faida kubwa

Hii huangusha sana wafanyabiashara wengi sana, ukiwaza kupata faida kubwa sana sio mbali biashara yako itakufa.
Waza kupata wateja wengi sana Na kama unavyojua Tanzania yetu watu wengi hupenda vitu vya bei ya chini ndo maana utaona watu wengi wananunua maji ya Mia yaliyofungwa Na kuacha ya miatano

6. Mazingira safi

Tengeneza Juisi yako katika mazingira ya wazi ukiimarisha usafi Na umakini mkubwa.

Nunua sare nyeupe pea kama sita Na vikofia Na grovuzi za kuvaa wakati wa kutengeneza Juisi,
Osha vifaa vyako vikae vikiwa safi hadi Juisi ionekane ilivyokaa kwenye kifaa mazingira yasafishwe Na kuwa mbali Na vitu hatarishi kama:
     -choo
     -shimo la taka
Usijifiche watu wakaanza kukutilia mashaka

Zalisha Juisi yako mapema sana kuanzia saa kumi hadi saa kumi Na mbili uwe umemaliza Na kupaki katika kipindi cha awali ili kuwezesha wasambazaji kupeleka Juisi kwenye masoko kwa wakati, yaani kufikia saa tatu masoko yote yamesambaziwa juisi.

7. Malipo mazuri kwa wasambazaji Na wafanyabiashara

Wape faida kubwa wasambazaji Na wafanyabiashara ili kupata molali ya kuendelea kuuza Juisi yako Na uzidi kuliteka soko.

8. Simamia mwenyewe

Nakwambia hivi simamia biashara yako kwa asilimia  Mia. Simaanishi ufanye kazi zote peke yako usije ukanielewa tofauti nasema simamia biashara yako mwenyewe usimpe kazi mtu mwingine halafu wewe ukajiweka kama bosi mkusanya pesa utalia mda sio mrefu.

Hakikisha kila unachokiwaza kinatekelezwa Na uliyemuagiza usicheke Na mtu kazini hapa pesa Mzee umewekeza, usijiondoe 😒😒😒😒😒

Jiunge Na group la Tuwemacho Enterprises la WhatsApp uzidi kujifunza kuhusu biashara mbalimbali kwa kubofaya hapa

Comments

  1. Nashukuru sana kwa ushauri mzuri na Allaah Akupeni barka ila naomba uniunge katika group la whatsapp kwenye namba hii 0784239393 please nitashukuru sana jina langu Mansur Ahmed

    ReplyDelete
  2. Asante kwa mwongozo mzuri Mungu awabariki naomba uniunge na mim kwenye group no yangu 0765304145

    ReplyDelete
  3. Na mm naomb uNiunge namba angu
    0763448140

    ReplyDelete
  4. Naomba uniunge kwenye group no 0655075823

    ReplyDelete
  5. Somo Zuri niunge nami nahitaji kuifanya iyo biashara 0742618425

    ReplyDelete
  6. Sawa niunge 0765047602

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Rangi za plate namba na maana zake Tanzania

Namna unavyoweza kutengeneza biashara kubwa kwa kuanzia mtaji mdogo wa shilingi 10000