Papa Francis amemvua madaraka Kardinali wa zamani, ikiwa ni tukio la kwanza kwa Kanisa Katoliki kuchukua hatua baada ya Mmarekani huyo, Theodore McCarrick kutuhumiwa kumbaka mtoto miaka 50 iliyopita, taarifa ya Vatican imesema jana. McCarrick, 88, ambaye alijitoa kutoka Taasisi ya Makardinali ya Vatican mwezi Julai, ni Kardinali wa kwanza duniani kutengwa kutokana na tuhuma za ngono. Mahakama ya Vatican ilimkuta na hatia ya kosa la kumbaka mtoto mwenye umri chini ya miaka 20, uamuzi uliothibitishwa na Papa mwezi huu, na hivyo hauwezi kupingwa zaidi, kwa mujibu wa taarifa hiyo. Ilisema McCarrick alipatikana na hatia ya “kuzini kinyume na amri ya sita kwa kufanya uzinzi na mtoto pamoja na watu wazima, na tatizo kubwa zaidi ni kutumia vibaya madaraka”. Taarifa hiyo inahitimisha kuanguka kwa aina yake kwa kardinali huyo aliyekuwa na ushawishi mkubwa na kumekuja kabla ya mkutano wa Vatican utakaofanyika Februari 21-24, ukihusisha maaskofu kutoka kila kona ya dunia kujadili namna ya kulinda ...