Miili 24 kuopolewa ikiwa imekufa

Waokoaji nchini Zimbabwe wameiopoa miili 24 ya watu waliokufa kwenye migodi miwili ya dhahabu iliyokumbwa na mafuriko mnamo siku ya Jumamosi. Watu wengine wanane wameokolewa. Kwa mujibu wa televisheni ya taifa, kuna hofu kwamba wachimbaji kadhaa walio nchini humo kinyume cha sheria bado wamekwama ndani ya migodi hiyo. Shughuli za uokozi bado zinaendelea katika migodi hiyo ambayo ilikuwa haitumiwi karibu na mji wa Kadona ulipo kilomita 145 kusini magharibi mwa mji mkuu Harare. Mnamo siku ya Ijumaa serikali ilitangaza juu ya kukwama kwenye migodi hiyo miwili wachimbaji wapatao 60 hadi 70.
chanzo www.aljazeera.com

Comments

Popular posts from this blog

Rangi za plate namba na maana zake Tanzania

Ijue zaidi biashara ya juice

Namna unavyoweza kutengeneza biashara kubwa kwa kuanzia mtaji mdogo wa shilingi 10000