Umekua ukiwaza juu ya mafanikio yako? jifunze jambo hapa




Mafanikio ni nini?
Nimekaa nakuwaza kwanini kila mmoja anataka kuafanikiwa? haijalishi watu wote hutamani kufanikiwa lakini waliofanikiwa bado si kila anaetaka kufanikiwa yaani leo huyu kafanikiwa huyu kaachwa na yawezekana wote walikua wanapambana kwa pamoja au yawezekana walifanya aina moja ya shughuri lakini katika suala la kufanikiwa huyu yuko juu huyu bado analia. 
kuna vitu kadha nataka nikushuhudie utaviangalia kwa mda wako utagundua jamboleo naanza na jambo moja 
MARAFIKI
Kati ya vitu ambavyo hujui vimekuweka hapo ulipo na kukufanya uwaze au usiwaze zaidi ufanikiwe au uzidi kua wakulialia  ni aina ya marafiki unaowashikilia na namna unavyoishi nao. Unaweza kusema huyu anajaribu kusema nini hebu endelea kusoma nikupe ushuhda utakusaidia kufungua akili yako ujue kua ninachokwambia kina ukweli ndani yake. 
katika ulimwengu wa marafiki kuna aina tofauti tofauti zaidi ya kumi,  leo nitakupa aina mbili tuu za marafiki siku nyingine nitakupa aina nyingine. Marafiki wa:
1.      kukatisha tamaa uwazapo jambo jipya
hawa ukija na jambo kama hajawahi kuliona, atakutisha tuu akikwambia rafiki yangu hapo usijaribu hufiki mbali na kuleta mifano ya watu walio jaribu kufanya kama wewe lakini walifeli,
Hasara yao
a.       hawawezi kuja na mfano wa mtu aliefanikiwa kwa kufanya kama wewe.
b.      Hawawezi kukuletea mawazo ya ni njia zipi zilisababisha wale waliofeli wakashindwa.
c.       Hawezi kukupa njia mbadala ya kufanya kupitia hilo wazo.
d.      Mara nyingi hawana jambo jipya la kufanya.
Faida yao: hukushitua kujua hatari zinazoweza kutokea baada ya kufanya ulichokua umekusudia hii ukusaidia usiende kichwa kichwa.
Ushauri wangu kwako: usikae mbali na marafiki wa aina hii tena jitahidi kuwashirikisha kila mara uwazapo jambo jipya la kufanya.
2.      Wenye kukutia moyo lakini hawawezi kuthubutu
Aina ya pili ya marafiki ni wale wanao kutia moyo kila uwaambiapo unataka kufanya jambo fulani linaloweza kukutoa ulipo. Hawa huona jambo unalowashirikisha katika hali ya mafanikio lakini ni hawawezi kukuza (kumodify) wao ukubali na kusema iko sawa lakini hawawezi kuona kinachoweza kutokea baada ya kufanya huona tu mafanikio na mara nyingi hua na mifano ya watu waliofanikiwa kwa mpango huo uliouwaza.
Hasara yao
Hasara yao kubwa ni
a.       hawawezi kukupa changamoto unazoweza kukutana nazo ukishaanza kazi hiyo wakiogopa wakisema utavunjika moyo.
b.      Mara nyigi ukiwashirikisha wanapiga chenga kuwa washirika wakiogopa wasipatwe na hasara (husubiri upige hatua kwanza huku wakiwa nyuma wanakutia moyo kwa maneno yao mazuri)
c.       Ni waoga wa kutoa maoni ya kukujenga zaidi
 Faida yao: Mara zote ni watu wanaotia moyo pale unapoonekana kukwama.
Ushauri wangu: usikae mbali na rafiki wa aina hii maana watakufanya usonge mbele usije kukata nia hata siku moja.
Marafiki hawa wawili ukiwakosa huwezi kutoka ulipo na kati ya makosa makubwa tunayoyafanya ni kuwakwepa marafiki wa kundi la kwanza na kuambatana sana na marafiki wa la pili. Nataka nikwambie hivi kukimbia changamoto sio kuepuka changamoto bali ni kwamba umerudi nyuma tuu huwezi kusonga mbele.
Fanya hivi: kaa na marafiki wako hao kwa uwiano mzuri ukiunganisha na lengo uliloleta, orodhesha mambo yote waliyo kushauri wote wawili mmoja kwa changamoto mwingine kwa mifano ya waliofanikiwa, kaa mwenyewe chunguza kundi waliofeli upate sababu ziorodheshe, angalia waliofanikiwa kwanini halafu orodhesha.
Ukishajumlisha yote jiulize unataka kufanya kwa mfumo gani mpya ambao haukuonekana pale? Halafu je umejipanagaje mpaka sasa? Kusanya nyenzo zako anza kazi nakushuhudia hivi utawapenda marafiki zako wote wa makundi mawili wakati unasonga mbele.
Katika mada nyingine nitakuonesha namna ya kukaa nao wakati unasonga mbele ili usije kuporomoka na kujutia.
JAMBO KUBWA USILOLIFAHAMU KATIKA MAFANIKIO
Kila hatua unayoipiga kwenda mbele kutoka kwenye shimo inahitaji uwe umeshiba una nguvu za kukutosha, hatua mia mbili kurudi ndani ya shimo hazihikuhitaji uwe umekunywa hata maji ni rahisi sana. Yaani ni rahisi kuugua kuliko kupona. 
kumbuka: 

  • mafaniko hayaji kwa siku moja.
  • mafanikio huwaijia wasiokata tamaa dhidi ya changamoto na kuzitatua.
  • mafanikio huwahitaji waliomaanisha kuyatafuta sio waliotamani kuyatafuta.

SONGA MBELE UKIZIANGALIA NA KUZILINDA HATUA ZAKO. 


Comments

Popular posts from this blog

Rangi za plate namba na maana zake Tanzania

Ijue zaidi biashara ya juice

Namna unavyoweza kutengeneza biashara kubwa kwa kuanzia mtaji mdogo wa shilingi 10000