CHA KUFANYA ILI KUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA KIFEDHA
2. WOGA
Haya sasa baada ya kupata wazo la kufanya. Watu wengi nimegundua baada ya kupata wazo la kibiashara hakuna hata mmoja anayekua mzembe kufanya utafiti, hili ni jambo muhimu sana katika aina yeyote ile ya biashara au utekelezaji wowote. Jambo ambalo linaloleta shida katika utafiti unaofanywa na mwekezaji ni asilimia kubwa ya wawekezaji hutegemea kupata taarifa nzuri zinazoongelea kitu wanachohitaji kuwekeza:
Kwanza kuona orodha za watu waliowekeza katika fursa hiyo na kufanikiwa.
Pili kukutana na orodha ya faida zinazotokana na uwekezaji huo tuu na si tofauti, rejea kwenye mfano wa uwekezaji wa kuku hapo juu.
Tatu kuona mchanganuo wa mapato makubwa yanayoweza kupatikana kwa mda mfupi endapo utawekeza katika fursa hiyo.
Lakini leo nataka nikwambie kitu usichokipenda kukisikia hakuna biashara yeyote inayoweza kukufanya uwe tajiri inaweza kukupa majibu ya aina hiyo. Ukiona hivyo ujue kuwa unafanywa tajiri kimawazo na unaishia kuwazia kuwa tajiri tuu miaka yote.
Watu wote waliofanikiwa kama wanavyoitwa kwa kishwahili kipya ‘waliotoka kimaisha’ wamepambana na zile nafasi zilizoachwa na watu wengine baada ya kuziona zina chanagamoto sana. Kwa maana nyingine ni hivi ili ufanikiwe lazima ushinde changamoto iliyojitokeza kuzuia watu wasipate huduma Fulani katika mazingira Fulani na wewe utokee kama mkombozi wao baaaaaasi hapo umeua!.
Woga husababisha mtu kushindwa kufanya alichokilenga chenye manufaa makubwa akiogopa
Kusindwa
kupata hasara
kuchekwa
Sasa nataka nikutolee mwiba uliokuzuia kutembea kufika mwisho wa safari yako ambayo hukupewa ramani ya mwisho wake ni lini au umbali wake ni upi bali unapewa ramani kidogo kidogo kila ufikiapo hatua fulani, mwiba huo ni woga, woga wako unaokufanya uhofie kuumia pindi utakapotoa mwiba, je utafika kwa kuchechemea huko? Acha woga toa mwiba songa mbele mguu utaoza huo ulazimike kukaa.
Ni hivi, kila penye mafanikio kuna changamoto kubwa sana ndo maana walio wengi hawajitokezi kupita hapo kwa kuwa barabara haijawahi kupitwa na mtu hivyo ina vigae miiba na kila aina ya changamoto.
Wewe kwakuwa unataka kufika mwisho wa safari yako nenda tu, songa mbele nenda kwa tahadhari na uongeze umakini ukiona mwiba ujue ni lazima ungeukuta maana ni njia ya kufikia mafanikio makubwa ambayo wengi wameogopa vikwazo hivyo toa mwiba songa mbele, ukiona kigae tafuta namna ya kukitoa halafu ongeza umakini ukitegemea kukutana na nyoka hatari pia mbele ya safari, usirudi nyuma ukaendelea kukaa ulipokuwa.
Fikiria nyuma ya msitu kuna mgodi wa dhahabu ukaangalia njia nyepesi ya kupitia kufika kule haipo ni vichaka tupu, utaacha kwenda? Au utasubiri mwingine apite kwanza atengeneze njia halafu upate upenyo unaopitika kirahisi? TAFAKARI kama hakuna njia inayopitika kufika huko na unajua kuna dhahabu ujue hakuna aliyewahi kwenda huko waweza kuwa wa kwanza, kama ulikuwa umebeba gunia moja ongeza matatu Zaidi ya kubebea dhahabu pindi utakapofika.
Kibaya ni kwamba kuna watu walikua hawajui kama kuna utajiri wa aina yeyote hivyo wakiona unakata njia jasho linakutoka watakuona kama mtu anaepoteza mda, aliyekoswa kazi au kichaa vile. Lakini wengine watakufuata kukuuliza ukiwaambia kuna dhahabu watacheka na kukwambia kule hakuna kitu chochote, kuna watu waliwahi kwenda hawakufika kabisa, huwa kuna wanyama wakali, wengine watakwambia bora ufanye kitu kingine hapo unapoteza nguvu.
Katika mafanikio yeyote usiangalie tuu yale ya watu waliyofanya wakafanikiwa, haikuwa rahisi kufanikiwa usidanganyike. Na kama umechagua njia hiyo ujue kuna ushindani mkubwa sana maana wengi wameshaona kuna mafanikio makubwa pale wakaamua kuwekeza.
Waliokutangulia kuwekeza wameshatengeneza jina na msingi wa huduma zao wewe unaanza.
NJIA ZA KUFANIKIWA KATIKA HUDUMA AMBAZO TIYARI ZIMEANZISHWA NA WAWEKEZAJI WENGINE KATIKA MAENEO YALEYALE NA YAMEONESHA MAFANIKIO.
Kumbuka kuwa walioanzisha huduma hiyo walianza kwa shida sana hadi kufikia walipo hivyo usiingie kichwa kichwa. Zingatia yafuatayo:
Angalia wapi wanapwaya, ili kupiga hatua na kuwa mtu mwenye kipato kikubwa kutokana na wazo ambalo limeanzishwa na wengine na linaonesha mafanikio ni kuangalia wapi panahitaji maboresho. Kipi wanakifanya, wanakifanyaje, unapaswa kuboresha wapi.
Angalia eneo jipya, Zaidi ya kug’ang’ania eneo lile lile ambalo lina watu tiyari waliotengeneza jina kubwa na kukutia changamoto sana jaribu kutoka nje kidogo ya pale ili kuweza kufanya huduma yako kwa ukaribu ukiwafikishia huduma karibu wale ambao walikuwa hawajapata hiyo huduma.
Angalizo:
Sehemu mpya sio lelemama, usifikirie kufika unawapa wazo lako halafu waone inafaa na kuzipokea huduma zako kirahisi utapaswa kuwa mvumilivu ukizingati vipengele tulivyoongelea kwenye kipengele cha wazo.
Comments
Post a Comment