NAWEZAJE KUFIKIA KIWANGO KIKUBWA CHA MAFANIKIO

1. Watu
Kuna watu wa aina mbili kuu utakaokutana nao wakati unajaribu kuwashirikisha katika kitu unachowaza.

Watu wanaokutia moyo
Hawa ni watu wazuri sana katika hatua yako ya kwanza unapaswa kukaa nao kwa karibu sana maana hukupa matumaini ya namna unavyoweza kufanikiwa kutoka katika mradi wako au biashara yako maana wakianza kukupigia faida inayotokana na biashara hiyo weeee!, watakupampu utatamani kuanza mda huo huo. Ila usiwe mtu wa haraka hapa maana bado kuna kikundi kingine muhimu hujakipata ambacho ni kikundi cha watu wa aina ya pili.
Uwapo na aina hii ya watu hakikisha unajipatia taarifa zote za maongezi yao kwa kuzingatia yafuatayo:
Wanonaje kama ukianzisha biashara hiyounaweza kupata faida kiasi gani?
Ni vitu gani hasa ukiviongeza katika biashara hiyo vinaweza kuleta faida sana katika biashara yako
Ni akina nani wamewahi kufanya biashara kama hiyo wamefanikiwa sana ni kitu gani kiliwasaidia, kwakua hawa ni watia moyo wanakuwa na orodha kibao ya watu waliotoboa kutoka katika biashara ya aina hiyo.
Usisahau kuwauliza kama kuna watu waliowahi kufanya shuguri kama hiyo lakini mambo yao hayaendi vizuri, hapa watakuwa hawana taarifa za ndani sana maana watu wa aina hii huangaika sana na waliofanikiwa ila walioshindwa hawana mda nao sana. Wata kusaidia kupata hata sababu za kwanini wale walianguka, kuuliza hapa inakusaidia katika hatua ya pili ya utafiti.
Watu wanaokukatisha tamaa (toxic people).
Hawa ni kati ya watu ambao husikilizwa sana na wawekezaji wengi sana, na kwa bahati mbaya watu hawa ni wengi sana kuwapata ni rahisi hivyo usihuzunike kila unayemshirikisha unakuta anakukatisha nia hawa ni wengi.
Kwanini ni wengi? Hawa ndio watu muhimu sana katika hatua yeyote ya uzalishaji maana ukufanya ujue changamoto zinazoweza kujitiokeza katika biashara yako na Mungu amewaweka kimakusudi ili wamusaidie motto wake kufikia maisha mazuri aliyowaahidi wale walio wake.
Watakupa maelezo mengi sana kuhusu kitu unachowaza kufanya na Zaidi watakushauri wakikuonesha kuwa njia uliyochagua ni ngumu sana hutafika mbali bora ubadirishe njia.
Nawewe unapopata bahati ya kukaa nao hawa usisahauu kupata taarifa zote muhimu kwa kuzingatia yafuatayo:
Ni hatari gani unaweza kupata pindi uanzishapo biashara hiyo.
Orodha ya watu waliowahi kuanzisha huduma hiyo mambo yao hayaendi.
Orodha ya watu walioanzisha huduma hiyo wameshindwa kabisa.
Bado usisahau kuwauliza juu ya mifano ya watu walioanzisha na wanaonesha mafanikio mazuri katika huduma. Kama ilivyo kwa kundi la watia moyo hawa pia hawanaga orodha ndefu ya watu waliofanikisha huduma hiyo bali wachache nab ado watakusaidia kupata mapungufu waliyonayo hao ambao bado wamesimama.
Usisahau kuwa watu wote waliofanikiwa huangaika na vitu viwili tu kukabiliana na changamoto zote pasipo kukata tamaa au kurudi nyuma, umakini na juhudi.

Comments

Popular posts from this blog

Rangi za plate namba na maana zake Tanzania

Ijue zaidi biashara ya juice

Namna unavyoweza kutengeneza biashara kubwa kwa kuanzia mtaji mdogo wa shilingi 10000