NAWEZAJE KUFIKIA KIWANGO KIKUBWA CHA MAFANIKIO?

Tamaa
Haya sasa umepata wazo ukapambana na woga ukashinda na kufanikiwa kupata maamuzi ya kuanza kitu kingine kinachoweza kuleta shida hapa ni tamaa. Tamaa huja hasa katika upande wa mafanikio tena sio tamaa tu maana asiyetamani sidhani kama anaweza kufanya jambo kwakuwa mambo mengi hutokea si tu kwa sababu ya ulivipenda mwanzo mara nyingine ulitamani baadhi ya vitu kwake na kujikuta umeanza kuviingiza kwenye akili na kujikuta unapenda sana hicho kitu na kuanza kuhitaji kukitekeleza.
Ila sasa kinacholeta shida ni kule kutamani kubaya (tamaa mbaya) ambako huja kwa mtu na kutamani kila kitu kiwezekane haraka haraka, yaani mtu anahitaji leo aanze leo hii aone matunda yake. Lakini mda mwingine mtu huipoteza fursa Fulani kwakupiga mahessabu ya mafanikio tuu na kuona anaweza kupata kiasi kidogo sana cha faida na kuamua kukimbia.
Je umewahi kujiuliza ni kitu gani kimefanya usiwe mbunifu na kuleta mabadiliko makubwa kwenye jambo unalolifanya? TAMAA, tamaa amekuwa adui mkubwa sana kusababisha udumavu wa akili kwa wawekezaji wengi na hii imekuwa inajitokeza pale mtu anapoanza kuzalisha. Uzalishaji unapoanza tu mwekezaji akavuna faida ya kwanza akili yake yote huiamisha kufikiria namna gani anaweza kuvuna sana na kuendelea kuvuna mara nyingi Zaidi.
Hii ndo hupelekea wawekezaji kutowalipa wafanyakazi wake kwa wakati akidai pesa haitoshi, kukopa benki ili kuongeza mtaji aweze kuvuna sana akijua pale sasa ndo penyewe penye faida kubwa, yaani hupiga mahesabu ya faida tu na kuvuna pesa huku akisahau kuwa pale panapoleta pesa wanaoleta pesa sio kwamba wanapenda kuleta pesa ni kwasababu wamefuata huduma tu hivyo ukiangalia tu namna ya kuvuna faida na kusahau kuangalia namna ya kuwahudumia wateja wako kwa kuangalia:
Kwanini wamechagua kuja kwako na si kwingine. Ukijua hilo utapaswa kuhangaika kuwahudumia Zaidi ya kuhangaika kuvuna kutoka kwao.
Vitu gani wanavilalamikia katika huduma yako unayofanya, ukijua hivyo vitu ndo utajua kuwa huduma yako imeanza kupatwa na homa inahitaji vipimo mapema ili ipate mseto mapema kabla ya kukupeleka mabali
Una idadi kiasi gani cha wateja unaowahudumia kwasasa hapo ndo unaweza kujua jedwali halisi la watu unaowahudumia na ni kiasi gani cha idadi halisi ya watu katika eneo hilo, na kwanini ni idadi hiyo umeipata.
Watu unaowahudumia ni wa kipato cha kati au cha juu au cha kawaida, na kama ni wa kipato cha juu kwa nini wa kipato cha chini hawaji kwako, hapo utafanikiwa kuboresha ili kuweza kuwahudumia watu wa aina zote pasipo kujali kipato chao kwa kutengeneza huduma kulingana na kipato cha wateja waliokuzunguka. Ndo maana kuna kifurushi cha saa 24, siku 3, wiki wezi na vifurushi hivyo vinatofautiana kulingana na matumizi.
Na Zaidi ni kwamba Tamaa hutia mtu upofu na kujikuta akijipenda yeye tu bila kujali mwingine yeyote yule, hapo kama na wewe umeshakuwa mlevi wa tamaa ujue unaelekea ICU tena maana utaanguka puuuuuuuu.
Cha msingi unachopawa kuzingatia ni kwamba hakikisha kazi yako inakuwa huduma ya kuwahudumia watu wengi ili iweze kuleta mafanikio makubwa.
Usisahau kuwa watu wote waliofanikiwa huangaika na vitu viwili tu kukabiliana na changamoto zote pasipo kukata tamaa au kurudi nyuma, umakini na juhudi.

Comments

Popular posts from this blog

Rangi za plate namba na maana zake Tanzania

Ijue zaidi biashara ya juice

Namna unavyoweza kutengeneza biashara kubwa kwa kuanzia mtaji mdogo wa shilingi 10000