Siri ya mafanikio
kama unafikiri kuna pesa inayopatikana kirahisi sana umepotea
Ukikaa usikilize mawazo ya makampuni ya kubeti ambayo hutoa tumaini la kulala maskini Na kuamka tajiri ujue unapoteza mda bure.
Huwezi kuwa mtu mwenye mafanikio bila kufanya kazi hakuna kitu kulicho rahisi katika ulimwengu huu labda Mwenyezi Mungu atoe ujumbe mpya tofauti Na ule wa utakula kwa jasho
Nakwambia hivi fuatilia uone kama kuna mtu aliyepiga hatua kimaendeleo atakwambia yeye alibahatisha kupitia sportpesa, mbet, Biko au Tatu Mzuka.
Mafanikio sio kubahatisha ni mambo yafuatayo yametendeka kwa uaminifu:
1. Uchaguzi
2. Uthubutu
3. Utayari
4. Uwajibikaji
5. Umakini
Kwanza chagua kufanya kazi sio kutegeshea kupata pesa.
Ukishachagua thubutu kufanya bila woga huku
ukiwa Tiyari kwa lolote changamoto ushindi, kuanguka Na kuinuka Na kusonga mbele bila kukata tamaa
Huku ukiwajibika mda wote bila kumwachia mwingine awajibike badala yako eti unamuachia sportpesa afanye kazi wewe uamke milionea 😀😀😀😀😀 utasubiri mpaka uzeeke.
Jambo lolote ukilifanya bila umakini tegemea kufeli tuu. Sikukatishi tamaa ila hutoboi ndugu yangu mfano umefungua kibanda unaemea unaweka kibanda kinajaa unauza yanaisha unaleta unauza hujui ongezeko hujui hasara hujui mategemeo baada ya mauzo halafu unaweka mtu anauza huna list ya umeleta nini unategemea nini baada ya mauzo
Nakwambia utaemea mpaka uzeeke maana unatengeneza faida Unafanya matumizi bila kujua umeingiza shilingi ngapi hujui unakula faida yote maadamu kibanda kimejaa ujue umekosa umakini utafanya kazi miaka mingi lakini maendeleo kidogo
Chukua hatua .
Haya mambo hataki hasira mimi mwenyewe bado napambana 😂😂😂😂😂😂
Karibu WhatsApp upate mambo motomoto Na mijadala muhiku kwa kubofya kwenye neno WhatsApp hapo chini
WhatsApp
Comments
Post a Comment