Matendo ya mpasayo kutenda au kuacha kwa muislamu (akhlaq)
Matendo ya mpasayo kutenda au kuacha muislamu [Moral
obligations (akhlaq)]
Hizi ni sharia ambazo kila muislam
azitimize, na sharia hizi zinaelekea kufanana na za kitabu cha agano la kale.
Baadhi ya sharia kama kutokuua, kutokuiba, kutokushuhudia uongo zote pia
zinapatikana katika quran na kitabu cha agano la kale, mfano wa sharia zile
zinazo patikana kwenye sura 17:31-39 zimebeba maneno mengi yanayopatika kweneye
agano la kale.
Ili tendo lolote kuhukumiwa ni zuri au
baya linategemea taratibu zilizowekwa ambazo zimegawanyika katika makundi
mawili; zile ambazo ni nzuri yaani zinazoonesha unyeneyekevu wa mwanadamu kwa
Mungu nazo huitwa mar’ufat na zile mbaya zinazoonesha uasi wa mwanadamu kwa Mungu
hizi huitwa munkarat.
Sehemu hiyo ya kwanza bado huigawa
katika sehemu nyingine tatu:
1. Fardh:
haya ni yale matendo ya lazima kwa kila muislamu kama kujitimiza nguzo
tano za uislam hapa mtu ataadhibiwa kwa kutokuzifuata na kufuata mafundisho ya
uislamu. Ndani ya kundi hili pia kuna zile zinaitwa wajib ambayo ni matendo
anayotenda muislam lakini haadhibiwi kwa kutokuyatenda pia kama kusaidia yatima
mwishoni mwa kipindi cha mfungo au kabla ya sala ya idd.
2. Marufat:
haya ni matendo ambayo yanasisitizwa kufanywa na hujulikana Zaidi kama mandub
yanasemekana kutokana Zaidi na uongezaji au upunguzaji wa mambo ya
kitamaduni ya zamani pamoja na misemo ya Muhammad. Mambo haya yanachukuliwa kua
mema kuyafanya kuliko kuyaacha mojawapo ni kuuona mwezi uliochomoza.
3. Mubah,jai’z
au halal: haya ni yale matendo ambayo muislamu huruhusiwa kufanya ila
ni ya hiari hutaadhibwa usipoyafanya.
Munkarat pia imegawanyika
katika sehemu kuu mbili
a. Haram:
ni matendo ambayo kila muislamu hapaswi kuyafanya na haya husababisha
adhabu kutoka kwa Mungu, haya hujumuisha dhambi kubwa kama kuvunja moja wapo ya
sharia, au kuvunja ahadi, kujiua, kulala na mwanamke aliye kwenye siku zake.
b. Makruh:
haya ni yale matendo ambayo adhabu yake sio kubwa sana lakini kwa muislamu
mwenye iman anaejua anachokifanya hapaswi kuyafanya kama kutamka sala ukiwa na
njaa, kuvunja mojawapo ya matendo madogo kwenye jamii, Zaidi ya haram na makruh kuna matendo ya kijumla ambayo muislam hapaswi kufanya kama
kuvunja mojawapo ya majukumu ambayo Muhammad alifanya. Maelezo haya yamehakikiwa vyema kutoka vyanzo zaidi ya kimoja kama inavyoonekana hapo chini. kama una elimu yoyote juu ya kilichoandikwa usiache ku comment hapo chini. pia follow kupata taarifa nyingine mpya.
VITABU NA KURASA ZA KUREJEA
Norlen, G. (2001). Islam and its World. Usa
River: Makumira Publications.
Comments
Post a Comment