Rangi za plate namba na maana zake Tanzania
TUJIFUNZE KIDOGO MAANA YA PLATE NAMBA NA RANGI ZAKE. 1. Kibao chenye rangi ya njano na namba inayoanza na herufi T Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kutumika kwa ajili ya shughuli binafsi. Kwa kiingereza inasemwa "private use". Magari yenye vibao hivi hayaruhusiwi kutumika kwa ajili ya biashara. 2. Kibao chenye rangi nyeupe na namba inayoanza na herufi T Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kwa ajili ya matumizi ya biashara. Kwa kiingereza inasemwa "commercial use". Mfano mzuri daladala au basi za kubeba abiria na taxi. 3. Kibao chenye rangi ya njano na namba haianzi na herufi T Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na taasisi ya umma au serikali. Hapa kuna makundi yafuatayo: (a) SU - shirika la umma, mfano vyuo vikuu vya serikali (b) SM - Serikali za Mitaa, mfano ni halmashauri (c) STK, STL, STJ - Serikali, mfano ni wizara 4. Kibao chenye rangi nyekundu na namba inayoanza na herufi DFP au DFPA Ki...

Comments
Post a Comment