NAWEZAJE KUFIKIA KIWANGO KIKUBWA CHA MAFANIKIO?
NAWEZAJE KUFIKIA KIWANGO KIKUBWA CHA MAFANIKIO?
Katika tafiti na uzoefu nilioweza kupata nimegundua kuwa kila mmoja anahangaika sana kuhakikisha anafanikiwa kimaisha, labda akiwaza kuwa tajili kama Fulani au akihitaji kufikia ndoto Fulani katika maisha yake. Lakini mambo siku zote yanakuwa hivi asilimia ndogo huweza kufikia ndoto zao na asilimia kubwa uendelea kuota pasipo kuamka usingizini, na asilimia kubwa kati ya wale waliofanikiwa kufikia ndoto zao au walio karibu kufikia ndoto zao hudumu kwa mda kisha huyumba au hufirisika.
Hapa nitaweka baadhi ya mambo ambayo usipoyaangalia kwa umakini yanaweza yakakufanya uendelee kuota tuu ndo pasipo kufikia hatima ya ndoto yako au kuisahau ndoto yako:
Wazo
Woga
Maamuzi ya wakati
Tamaa
1. WAZO
Mara nying watu hutafuta wafanye nini yaani ni kitu gani wawekeze kwacho. Na hili limekuwa tatizo linalosumbua watu wengi sana kufikia hadi asilimia tisini. Hii imepelekea baadhi ya watu kuweka dau kubwa ili kununua wazo la kibiashara kuytoka kwa wabunifu wa mawazo ya kibiashara na kisha kuwekeza kiasi kikubwa sana cha fedha ili kuzalisha kupitia wazo hilo.
Hii mara nyingine imekuwa ikiwatoa watu baadhi na kuwafanya matajiri huku wengine wakijikuta wanafirisika na kuanguka kiuchumi.
Yawezekana hata wewe umekuwa miongoni mwa waathirika wa tatizo hili, ukijiuliza mara kwa mara Je? Nifanye nini ili nifanikiwe kimaisha? Na mda mwingine mtu aliyepiga hatua kidogo hasa waajiliwa huumiza sana kichwa na kujiuliza nifanye nini ili nipige hatua Zaidi na kujipatia utajiri?.
UTATUZI UNAOWEZA KULETA MSAADA
Labda kabla ya kuangalia utatuzi wa namna gani mtu anaweza kupata wazo na kuliendesha nikupe siri moja ambayo waweza kuwa uliwahi kuisikia ila huijui au hujawahi kuijua kabisa. Kila mmoja katika ulimwengu huu ameumbwa kufanikiwa na kuishi kwa furaha kabisaaaa, hivyo basi kutokana na ukweli huo kila mtu Mwenyezi Mungu amemuumba na kitu cha ziada ambacho kupitia hicho yeye ataweza kufanikiwa.
Kufanikiwa na kutokufanikiwa kwako kunategemea na matumizi ya hicho ulichopewa katika kutimiza hazima ya kufanikiwa kewako. Sasa nataka nikupe njia unazoweza kuzingatia ili kufikia mafanikio yako.
Kwanza acha kupoteza kiasi cha fedha ulichonacho kutafuta wazo la kibiashara ili kuwekeza, maana kufanya hivyo mimi nakufananisha na mtu mmoja aliyefunagasha safari na kwenda kwa mganga wa kienyeji aliyekuwa anakaa kijiji cha mbali ili ampe dawa ya kufanikiwa kuwa tajiri na wakati mganga anakaa chini ya mti mkubwa wa mbuyu. (hapo utakuwa unacheza mchezo wa bahati nasibu) kwanini nasema hivyo ? chukulia mfano huu:
Mtu mmoja alipewa wazo la biashara kutoka kwa mbunifu aliyegundua kuwa mteja wake anapenda sana mafanikio ya haraka kwa kumwambia hivi: “Nipe million moja nitakupa wazo la biashara ambalo litakuhitaji uwekezaji usiofikia hata laki tatu, baada ya kulipa kiasi cha fedha akapewa wazo kama ifuatavyo: jenga banda dogo lenye uwezo wa kuchukuwa kuku watano, nunua kuku wanne mitetea waliofikia umri wa kutaga na mmoja jogoo mwenye umri wa kurutubisha.
Nunua chakula cha kuku kwa gharama y ash. 69000 hii utanunua pumba gunia moja kwa makadirio ya sh 20000 kwa kilo 70, mashudu ya alizeti kilo 15 ambayo haiwezi zidi 10500 kwa makadirio y ash 700 kwa kilo, paraza ya mahindi kilo 25 kwa makadirio ya 700 kilo ongeza kilo 25 za chakula kingine kama mtama kwa bei ya 700 makadirio ya juu utafikisha kilo mpaka 135 ambapo kuku mmoja hula mpak gram 130 kwa siku hivyo kwa siku mbili kuku wako watano watakula mpaka kilo 1.3 hapo utaweza kuwahudumia kuku wako kwa miezi mpaka sita.
Tumia 80000 kununua kuku yaani 15000 mitetea na 20000 jogooo jumla 149000.
Banda lako dogo linaloweza kukugharimu mapaka elfu 60000 la kuhamishika. Jumla 209000
Haya kuku hawa wakitaga mayai kumi wote wakaatamia utapata mayai 40 waatamie na kutotoa vifaranga 6 kwa kila mmoja wastaniutakuwa na vifaranga 24 ukiwatunza vizuri wanakua wote basi wakifa 10 utakuwa na vifaranga 14 ndani ya miezi miwili waachishe mama zao na uwatunze wenyewe ili kuruhusu mama zao kutaga tena ambapo mwezi wa tatu wanaweza kutaga tena kwa mwendo uleule utapata kuku wengine 14 jumlisha 14 =24 jumlisha 5 =29 kwa miezi sita mwezi wa saba wale 14 wa mwanzo wawepo mitettea 10 na jogoo 4 wanaweza kutaga pamoja na hao 4 kwa hiyo utakuwa na kuku 14 wanaoweza kutaga ukifuata njia kama za awali mwezi wa kumi na mbili wa ufugaji utakuwa na kuku 14 X 14= 169+29=198 hao kuku ni ndani ya wiki tisa hadi kumi tu kwa makadilio ya chini sasa hadi kufikia mwisho wa mwaka unaweza kupanua sana mabanda maaana ni hatari sana utagaji utakao fuata.
Ukiangalia kwa haraka utahisi hapa ndo penyewe utakimbia ukiona fursa kubwa ya kuwa tajiri lakini sasa kumbe kuna mambo ambayo hukuyajua katika fursa uliyoenda kuwekeza ukifikiria kupitia hilo utakuwa tajiri (self made millionaire)
Sitaki nikwambie ukinunua wazo haliwezi kukufanya uwe tajiri la hasha! Kuwa Na wazo ni hatua moja Na kufanikisha wazo ni Jambo jingine tofauti.
Hasara kubwa ya kupewa wazo ambalo linaweza kukutoa tena kwa kulinunua kwa gharama kubwa ukiwa Na matumaini makubwa sana ni kujikuta umewekeza kila kitu pasipo
elimu
mapenzi
Moja Elimu ya kutosha si tu ya vitabu bali uzoefu kutoka kwa wawekezaji wengine kwa kuangalia waliofanikiwa Na walioanguka Na wanaoyumba ni muhimu sana.
Pili Mapenzi ya kile unachokifanya ni msingi mkubwa wa mafanikio waliofanikiwa si kwasababu wanatafuta tuu pesa ila ni kwa Sababu wanapenda kile wanachokifanya Na mara zote huwaza sana kuhusu kazi yao karibia masaa yote
Na zaidi huiona kazi yao kuwa ni huduma Na hupata sana hofu pale wanaposhindwa au kuwachelewesha wanaowahudumia Na si kuwaza hasara tu wanazozipata. Hapa wawekeaji wengi wamekuwa na presha juu ya kupata hasara, kutokupata kiasi kizuri cha fedha walichokitegemea katika uwekezaji wao.
Jambo hili hupelekea muwekezaji kupandisha gharama, kukwepa kodi, kutowalipa waajiriwa, haya yote ilia one kama atapata faida kubwa kutoka katika bisha yake jambo ambalo hupelekea mambo yafuatayo:
Huduma mbovu kutoka kwa waajiriwa kwenda kwa wateja
Kupigwa faini za mara kwa mara na kuoga ili asipelekwe mahakamani
Kupoteza kiasi kikubwa cha wateja kutokana na huduma mbaya wanazozipata
Kupoteza nguvu kazi kutoka kwa watu aliowaajiri kutokana na kutolipwa vizuri mishahara
Kupigwa ganji na wafanyakazi kitu kinachoweza kuchangiwa na hali halisi yakutolipwa.
Nataka nikwambie hivi wazo la kufanikisha hatima yako yote ya maisha unalo wewe hapo cha msingi angalia kitu unachokipenda sana wekeza Na usikione kama kazi tu kifanye kuwa huduma watu wengi hupenda kuhudumiwa zaidi ya kuuziwa tuu.
Kama ni kufuga fuga kile unachokipenda sana nafsi itakipenda utapatwa na huruma pale linapotokea tatizo utahangaika ili kunusuru uhai wa mifugo hiyo na si kuwaza hasara
Nataka nimalizie katika kipengele hicho kuwa “kufanikiwa kunakaa mbali sana ya hasara hivyo ukitaka kufanikiwa ongeza hasara mara mbili ili ufike haraka” Ukitaka kuthibitisha hilo kafanye utafiti kwa waliofanikiwa waliokaribu yako waulize walipitia wapi?
Usirudi nyuma songa mbele angalia pale panapoleta shida tafuta utatuzi Zaidi ukiwaza kuwahudumia watu wengi zaidi.
Lenga kukuza huduma si kuwa kubwa kimafanikio ya kifedha ila iwafikie wengi Zaidi na hiyo iwe furaha yako kuona unawahudumia watu wengi Zaidi.
Usilenge kazi yenye makusanyo makubwa ya faida bali yenye makusanyo ya kawaida ya faida ila ikiwalenga watu wote wa hali ya chini, ya kati, na ya juu.
Kadri unavyowahudumia wateja wako jaribu kuangalia mahitaji yao wote ukijaribu kugawanya huduma katika makundi yote ya watu wenye kipato cha chini, cha kati, na kipato cha juu. Usiuze kwa wale wa jumla tuu lenga kuuza hata wa rejareja, usiuze bidhaa za kiwango kikubwa cha fedha tuu bali punguza saizi wauzie na wa kipato cha kawaida pia hapa ndipo utajiuliza kwanini Vodacom wana hadi vocha za 200.
Usianzie juu anzia chini yaani anza kidogo kidogo ukipanua taratibu itakusaidia kuzijua changamoto ndogondogo zisizo Na hasara kubwa ukianzia juu ukianguka ni puuu ICU.
Kaa karibu na huduma yako wahudumie watu Na panua kulingana Na mahitaji. Usijifanye bize ukaweka kazi yako kwa mtu mwingine asilimia mia, je? Una uhakika gani huyo ana malengo kama ya kwako?
Fuatilia sehemu zote za za huduma yako Na angalia wapi kuna tundu ziba. Hapa utagundua kwanini makampuni ya uzalishaji kama mtibwa sugar, kagera sugar wameajiri hadi mtu wakuzunguka kuangalia ni kiasi gani cha miwa imedondoka njiani wakati wa usafirishaji wake, huyu utaona anasaga mafuta tuu akizungukazunguka.
Ukipanua huduma igawe katika vitengo ili uweze kuimudu. Ukichanganya vitengo watakuchanganya utashindwa kujua hasara zinatokea wapi.
Waweke bize waajiliwa wako usiwakutanishe pamoja yaani angalia mda wanaoweza kutumia kazini serious ukiisha waruhusiwe kuondoka hii itakusaidia kupunguza kiasi kikubwa cha fedha ambacho mtu anaweza kulipwa kwa kukaa kazini kumbe kazi yake ilikuwa ndogo kamaliza mapema.
Comments
Post a Comment