NAWEZAJE KUFIKIA KIWANGO KIKUBWA CHA MAFANIKIO?
3. Maamuzi
Katika kipengele kilichopita tumeona woga unavyokwamisha mtu kupiga hatua kuelekea mafanikio aliyoyakusudi, sasa hapa tutazidi kuona jinsi uamuzi wako ndio suluhisho kubwa la maisha yako. Mafanikio yote hutegemea maamuzi yako kufanikiwa au kutofanikiwa hutegemea uamuzi wako mwenyewe, maamuzi huweka malengo, malengo hutoa mwelekeo na mwelekeo huchochea kujituma na kujituma huchomoza mafanikio halisi. Lakini katika kuamua hapo ndipo watu wengi hujikuta wakifeli na kuaanza kumtafta mchawi wa maendeleo yao pasipo kujua kua maamuzi yao ndio yamewafelisha.
Mtu mmoja huamua kufanya kazi kwa bidii, mtu mwingine huamua kuiba, mtu mwingine huamua kwenda kwa waganga ili apate pesa akiwa amekaa, hawa wote mafanikio yao yanakuja au yanaharibika kutokana na maamuzi yao. Hivyo suala la maamuzi ndio muhimili mkubwa wa mafanikio uliyonayo au kushindwa kwako kufikia maono uliyonayo.
Kwakua tulishajua kuwa kila mmoja ana uwezo wa kuanzisha wazo na kufikia mafanikio, sasa tuangalie uamuzi namna gani unaweza kufanywa ili kufikia malengo yako unayoyawaza.
Kwanza, kumbuka kujali mda: mda ni jambo la msingi sana kuliangalia pale unapofanya maamuzi yako. Wengine ukiwauliza mbona hili hukufanya anakwambia mda haukutosha, mwingine atasema mda bado, mwingine atasema subiri kwanza. Kutokana na hayo utagundua kuwa Tatizo sio mda maana sote tumepewa masaa 24 tatizo ni ‘uamuzi’.
Mtu yeyote mwenye malengo na kujua anaelekea wapi (mwelekeo) akijituma kwa nguvu zake zote huwezi kumzuia kufikia mafanikio. Katika uamuzi hatuangalii uamuzi tu bali uamuzi wa busara, uamuzi wa busara hujali mda. Fikiria mgonjwa wako yupo ICU anahitaji kufanyiwa upasuaji sasa lakini unahitajika usaini kwanza, je utahitaji kukaa kwanza kupata uamuzi wa kukubali kutoa saini ili mtu afanyiwe upasuaji? Hapo uamuzi wako kwa wakati ndio utawezesha kuokoa au kutookoa uhai wa mgonjwa wako.
Kama kuna kitu ulikuwa hujui maisha yako yapo ICU uamuzi wako ndio utasababisha kupona au kutopona kwako. Ili kufikia mafanikio unapaswa kuwa na uamuzi unaojali mda, sio kitu kimoja unawaza kukifanya lakini unakaa Zaidi ya mwaka unawaza tu namna ya kufanya pasipo kutoa uamuzi. Utaishia kuwaza tu ndugu yangu wenzako wanazidi kupiga hatua kwenda mbele. Hizo changamoto unazoziona na kushindwa kutoa maamuzi ya kuanza, je unasubiri lini zijiondoe uanze?
Haya ni baadhi ya mambo yakuzingatia katika kufanya jambo linalohitaji kutolea maamuzi
Ili kufikia tamati ya uamuzi wako katika jambo linaloamua hatima ya maisha yako fanya yafuatayo:
Wekeza akili yote na mda katika jambo unalohitaji kufanya, hii itakusaidia kufikia maamuzi kwa wakati.
Fanya utafiti wa kina katika kile unachohitaji kutolea uamuzi hii itakusaidia kupata uamuzi wa busara na kuepuka kujitia uamuzi wako.
Kwakua wakati unawaza kuanzisha huduma ya uzalishaji uliona unaweza kupata faida kubwa, sasa hakikisha unapata taarifa zote zinazoweza kuleta hasara katika huduma unayotaka kuanzisha, hii itakusaidia kupata maamuzi mazuri ya namna ya kujitatua changamoto zinazoweza kusababisha hasara katika huduma yako pindi utakapoianzisha.
Mara zote iko wazi kuwa katika dunia hakuna kitu kipya, hivyo tunaamini kila unachowaza kuna mwingine amefanya kama sio hapa basi ughaibuni. Hivyo basi fuatilia kuhusu watu wengine waliokutangulia katika huduma hiyo na uangalie ni wapi wamefanikiwa na ni wapi wameshindwa, hii itakusaidia kupata uamuzi wa ni wapi uongeze katika huduma yako ili ilete mvuto.
Kumbuka uamuzi wako wa wakati ndio utakufanikisha kutoka ulipo.
Uamuzi wako wa haraka katika usimamizi wa shughuri yako ndio utasaidia biashara yako isiyumbe, sio unagundua kuna sehemu inasababisha hasara kwenye biashara yako, au kipato kinachoapatikana hakiendani na matumizi yako ya kawaida yaani hujui kiasi kingine kinaenda wapi au uzalishaji ni kama huleti mafanikio kadri ya uwekezaji wako, halafu unachukua mda mrefu kufanya maamuzi. Zaidi wasiliana nasi kupitia whatapp number +255762125819.
Comments
Post a Comment