NAWEZAJE KUFIKIA KIWANGO KIKUBWA CHA MAFANIKIO?

Mambo ya msingi ambayo waliofanikiwa huwafanya wazidi kufanikiwa.
Je mambo gani watu waliofaniukiwa na kuwafanya wafanikiwe? Na mambo gani huwa tofauti na wale ambao bado hawajafanikiwa?
Ndoto
Watu waliofanikiwa kwanza huwa na ndoto kubwa yaani huwaza mbali (hulenga mbali). Mtu mweny endoto kubwa siku zote hupambana kuzifikia ndoto zake ndio maana Yusuph alikuwa na ndoto ya kusimamisha mganda wake kati kati ya miganda ya ndugu zake na miganda ya ndugu zake kuinamia mganda wake. Mwanzo 37:7 hivyo ndivyo watu waliofanikiwa huota na kuamini ndoto zao huamini kusimama katikati ya walioshindwa na wao kuibuka washindi katika mambo yao. Ukiwaza juu ya mafanikio siku zote utafanikiwa tuu ukiwaza juu ya kushindwa hata usijisumbue wewe umeshindwa tuu.
Hukaza mwendo siku zote.
Zaidi ya ndoto kitu kingine cha tofauti kwa watu waliofanikiwa ni kukaza mwendo siku zote. Hawa ni watu ambao hawakai wakasubiri miujiza ijitokeze bali husimama imara na kusonga mbele ili kusababisha ndoto zao kutimia sio kukaa na kusubiria.
Watu wengine huwa na ndoto na ndoto zao huishia kuitwa ndoto, huwaza kujenga majumba makubwa, kumiliki magari na kuwa matajiri ila hawathubutu kusonga mbele kukabilia changamoto ili kubadirisha ndoto zao kuwa kweli. Ukimuangalia Yusuphu alipopata fursa ya kukaa nyumbani kwa mfalme alihakikisha anafanikisha yote aliyopewa na mfalme usifikiri ilikuwa rahisi ila alipambana ili siku moja afikie ndoto zake wala hakufanya papara. Mwanzo 39:3.
Waliofanikiwa siku zote hawakati tamaa
Ukisoma historia za watu waliofanikiwa utagundua namna gani haikuwa rahisi kwao kufanikiwa hatutaenda mbali kafuatilie Abdul Nasibu maarufu kama Diamond wa kipindi cha kukaa mtaani akipiga vibarua na kupata pesa ya kuingia studio hadi leo hii kuwa msanii anaeweza kwenda nchi za nje kufanya nyimbo na wasanii wakubwa sio rahisi kabisa. Wengine kafuatilie akina Jack ma muanzilishi wa alibaba namna walivyoona anafanya upuuzi tuu na hawezi kufika mbali lakini yeye akapiga mwendo na leo hii ni miongoni mwa watu waliotengeneza e-commerce moja kubwa sana. Ukikata tamaa ujue huwezi kufika mbali ukiangalia unapoelekea kwa macho yako au ya wengine huwezi kuona ispokuwa kwa macho ya ndani tena ndani yako tu ndo huweza kuona mbele unapoenda songa mbele achana na maneno ya waoga. Kaza mwendo vunja changamoto fikia malengo! Watu waliofanikiwa siku zote hawakimbii hata ulete bastola uiweke kichwani hawatoki mzee pale walipowekeza akili yao hawarudi nyuma wala hawakati tamaa.
Mara zote hutegemea majibu mazuri
Ukiwaangalia waliofanikwa wote ni watu ambao huwaza na kuona mafanikio mbele yao mara zote, pindi wanapofanya mambo yao yakaenda mrama hujua kua ni changamoto tu hutafuta njia ya kuzitatua na kusonga mbele, jambo la msingi hutembea kwa tahadhari hapo baadae kuepuka kurudia changamoto zile zile walizokutana nazo hapo awali.
Waangalie akina Mohamed Dewji na ujiulize kipindi wanaanza uzalishaji walifikiria kwamba hawatauza baadae katika nchi hii yenye uchumi ambao hata haujafikia uchumi wa kati, je walizalisha na kuanza kuuza mara moja kwa kasi? Vipi Bakhressa ambaye inasemekana alikuwa anashona viatu na kufanya biashara ya viazi na hakuweza kusoma elimu ya sekondari kutokana na maisha ya nyumbani kwao kua magumu.
Huziamini ndoto zao
Watu waliofanikiwa siku zote huziamni ndoto zao, ni lazima kuziamini ndoto zako usipofanya hivyo unahisi ni nani anaweza kufanya hivyo?
Ni lazima uziamini na kuzilinda ndoto zako kama ilivyo kwa kila mtu hupatwa usingizi kwa wakati wake tofauti tofauti na mwingine ndivyo kila mmoja huwa na ndoto tofauti pia huwa na maono tofauti pia na hutofautiana katika kupambanua mambo.
Ziamini ndoto zako! zipambanie ndoto zako! Zilinde ndoto zako! Usikubali kunyanganywa ndoto zako!.

Comments

Popular posts from this blog

Rangi za plate namba na maana zake Tanzania

Ijue zaidi biashara ya juice

Namna unavyoweza kutengeneza biashara kubwa kwa kuanzia mtaji mdogo wa shilingi 10000