Posts

Rangi za plate namba na maana zake Tanzania

Image
TUJIFUNZE KIDOGO MAANA YA PLATE NAMBA NA RANGI ZAKE. 1. Kibao chenye rangi ya njano na namba inayoanza na herufi T Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kutumika kwa ajili ya shughuli binafsi. Kwa kiingereza inasemwa "private use". Magari yenye vibao hivi hayaruhusiwi kutumika kwa ajili ya biashara. 2. Kibao chenye rangi nyeupe na namba inayoanza na herufi T Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kwa ajili ya matumizi ya biashara. Kwa kiingereza inasemwa "commercial use". Mfano mzuri daladala au basi za kubeba abiria na taxi. 3. Kibao chenye rangi ya njano na namba haianzi na herufi T Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na taasisi ya umma au serikali. Hapa kuna makundi yafuatayo: (a) SU - shirika la umma, mfano vyuo vikuu vya serikali (b) SM - Serikali za Mitaa, mfano ni halmashauri (c) STK, STL, STJ - Serikali, mfano ni wizara 4. Kibao chenye rangi nyekundu na namba inayoanza na herufi DFP au DFPA Ki...

Siri ya mafanikio

kama unafikiri kuna pesa inayopatikana kirahisi sana umepotea Ukikaa usikilize mawazo ya makampuni ya kubeti ambayo hutoa tumaini la kulala maskini Na kuamka tajiri ujue unapoteza mda bure. Huwezi kuwa mtu mwenye mafanikio bila kufanya kazi hakuna kitu kulicho rahisi katika ulimwengu huu labda Mwenyezi Mungu atoe ujumbe mpya tofauti Na ule wa utakula kwa jasho Nakwambia hivi fuatilia uone kama kuna mtu aliyepiga hatua kimaendeleo atakwambia yeye alibahatisha kupitia sportpesa, mbet, Biko au Tatu Mzuka. Mafanikio sio kubahatisha ni mambo yafuatayo yametendeka kwa uaminifu: 1. Uchaguzi 2. Uthubutu 3. Utayari 4. Uwajibikaji 5. Umakini Kwanza chagua kufanya kazi sio kutegeshea kupata pesa. Ukishachagua thubutu kufanya bila woga huku ukiwa Tiyari kwa lolote changamoto ushindi, kuanguka Na kuinuka Na kusonga mbele bila kukata tamaa Huku ukiwajibika mda wote bila kumwachia mwingine awajibike badala yako eti unamuachia sportpesa afanye kazi wewe uamke milionea 😀&#...

Ijue zaidi biashara ya juice

Leo tunaendelea Na biashara ya juice changamoto na namna gani unavyoweza kuimudu Changamoto zinazoweza kupatika katika biashara ya juisi Kuharibika : Kutokana Na kuwa juisi unayotengeneza haina kemikali yeyote iliyoongezwa ili kuitunza hivyo huweza kuharibika pindi ikikaa kwa mda wa zaidi ya saa 24. Kumbuka Juisi atakayopeleka mteja aliyesambaziwa ataiweka kwenye jokofu lake Na kawaida ya wafanyabiashara hawezi kuwasha jokofu mda wote hivyo uhakika wa Juisi kukaa kwa mda mrefu unakuwa mdogo. nini kifanyike 1. Usitengeneze Juisi nyingi wakati unaanza tengeneza Juisi kidogo huku ukizidi kupanua masoko yako. Hii itakusaidia kuzijua changamoto zinazokupata zikiwa kidogo Na kuzitatua bila ya kupata hasara kubwa sana. 2. Weka Juisi kidogo kwa mfanyabiashara wakati mnaanza biashara usizidi pakiti tano kwa sehemu inayochangamka Na pakiti tatu kwa duka linadolola. 3. Fungasha Juisi za bei ya chini kuanzia miatatu Na miambili ikiwezekana Na za Mia Mia  usifungashe za miatano maana...

Namna unavyoweza kutengeneza biashara kubwa kwa kuanzia mtaji mdogo wa shilingi 10000

JUICE ZA MATUNDA, Matunda ya elfu kumi hasa maembe na maparachichi unaweza kutoa hadi lita kumi za juice safi tunakadiria lita moja ni kutoa glass tano au nne za juice hivyo basi kwenye lita kumi unaweza kupata bilauri 40 ambazo ni sawa na elfu ishirini kwa bei ya 500 kwa bilauri moja ukitoa matunda,sukar na vigras unafaida elfu tano, Hapa unaweza kujiongeza usiwaze kiudogo udogo. Tengeneza channel ya wasambazaji unaweza kuanza Na mmoja, kabla ya yote pita mwenyewe kwenye vibanda ongea Na wauzaji wenye Majokofu unwaachia juice kidogo kidogo kama umeacha kumi anachukuwa moja kama umeacha tano unampa nusu ni mfano tu . Halafu unakuwa unazalisha nakuweka kwenye vibanda panua soko taratibu. Unaweza kuwa unapak kwenye mifuko kama maji ya kandole halafu unaweka ya 200 utauza sana

Kuondoa app zilizotengenezwa moja kwa moja kwenye simu Na kuzuiwa kuondolewa

Mara nyingi watu tumekuwa tukitamani kuondoa baadhi ya app zilizopo kwenye simu lakini ukigusa ili kuondoa hazileti option ya uninstall hivyo kukufanya tukae Na app ambazo hatyzitaki Lakini kwakuwa teknolojia ipo mikononi mwetu watu wameiona hiyo kuwa kama fursa baada ya kugundua hitaji la watu. Wameamua kutengeneza app anayotuwezesha ku root simu yako Na kuamua kuitumia bila vipigamizi vya walioitengeneza. Kuna app nyingi wametengeneza lakini mimi nakuja Na app moja makini sana inayojulikana kama kingoroot App hii inakuwezesha kuondoa app zote zinazokusumbua baada tu ya kuroot simu yako UNACHOHITAJI KUFANYA Pakua app ya kingoroot I run kwenye simu root simu yako halafu nenda kaondoe app usiyoipenda kwenye app yao itakayojiweka automatic kwenye screen Unaweza kuipata app hiyo kama unapata shida kupitia WhatsApp namba +255762125819 Na kama unakwama usisite kuuliza

NAWEZAJE KUFIKIA KIWANGO KIKUBWA CHA MAFANIKIO

1. Watu Kuna watu wa aina mbili kuu utakaokutana nao wakati unajaribu kuwashirikisha katika kitu unachowaza. Watu wanaokutia moyo Hawa ni watu wazuri sana katika hatua yako ya kwanza unapaswa kukaa nao kwa karibu sana maana hukupa matumaini ya namna unavyoweza kufanikiwa kutoka katika mradi wako au biashara yako maana wakianza kukupigia faida inayotokana na biashara hiyo weeee!, watakupampu utatamani kuanza mda huo huo. Ila usiwe mtu wa haraka hapa maana bado kuna kikundi kingine muhimu hujakipata ambacho ni kikundi cha watu wa aina ya pili. Uwapo na aina hii ya watu hakikisha unajipatia taarifa zote za maongezi yao kwa kuzingatia yafuatayo: Wanonaje kama ukianzisha biashara hiyounaweza kupata faida kiasi gani? Ni vitu gani hasa ukiviongeza katika biashara hiyo vinaweza kuleta faida sana katika biashara yako Ni akina nani wamewahi kufanya biashara kama hiyo wamefanikiwa sana ni kitu gani kiliwasaidia, kwakua hawa ni watia moyo wanakuwa na orodha kibao ya watu waliotoboa kutoka k...

NAWEZAJE KUFIKIA KIWANGO KIKUBWA CHA MAFANIKIO?

Mambo ya msingi ambayo waliofanikiwa huwafanya wazidi kufanikiwa. Je mambo gani watu waliofaniukiwa na kuwafanya wafanikiwe? Na mambo gani huwa tofauti na wale ambao bado hawajafanikiwa? Ndoto Watu waliofanikiwa kwanza huwa na ndoto kubwa yaani huwaza mbali (hulenga mbali). Mtu mweny endoto kubwa siku zote hupambana kuzifikia ndoto zake ndio maana Yusuph alikuwa na ndoto ya kusimamisha mganda wake kati kati ya miganda ya ndugu zake na miganda ya ndugu zake kuinamia mganda wake. Mwanzo 37:7 hivyo ndivyo watu waliofanikiwa huota na kuamini ndoto zao huamini kusimama katikati ya walioshindwa na wao kuibuka washindi katika mambo yao. Ukiwaza juu ya mafanikio siku zote utafanikiwa tuu ukiwaza juu ya kushindwa hata usijisumbue wewe umeshindwa tuu. Hukaza mwendo siku zote. Zaidi ya ndoto kitu kingine cha tofauti kwa watu waliofanikiwa ni kukaza mwendo siku zote. Hawa ni watu ambao hawakai wakasubiri miujiza ijitokeze bali husimama imara na kusonga mbele ili kusababisha ndoto zao kutimia...