NAWEZAJE KUFIKIA KIWANGO KIKUBWA CHA MAFANIKIO
1. Watu Kuna watu wa aina mbili kuu utakaokutana nao wakati unajaribu kuwashirikisha katika kitu unachowaza. Watu wanaokutia moyo Hawa ni watu wazuri sana katika hatua yako ya kwanza unapaswa kukaa nao kwa karibu sana maana hukupa matumaini ya namna unavyoweza kufanikiwa kutoka katika mradi wako au biashara yako maana wakianza kukupigia faida inayotokana na biashara hiyo weeee!, watakupampu utatamani kuanza mda huo huo. Ila usiwe mtu wa haraka hapa maana bado kuna kikundi kingine muhimu hujakipata ambacho ni kikundi cha watu wa aina ya pili. Uwapo na aina hii ya watu hakikisha unajipatia taarifa zote za maongezi yao kwa kuzingatia yafuatayo: Wanonaje kama ukianzisha biashara hiyounaweza kupata faida kiasi gani? Ni vitu gani hasa ukiviongeza katika biashara hiyo vinaweza kuleta faida sana katika biashara yako Ni akina nani wamewahi kufanya biashara kama hiyo wamefanikiwa sana ni kitu gani kiliwasaidia, kwakua hawa ni watia moyo wanakuwa na orodha kibao ya watu waliotoboa kutoka k...