FAIDA YA NGUVU ZILIZOMFUFUA YESU
Bwana Yesu asifiwe milele! Faida nyingine unayotakiwa kunufaika nayo unapokuwa unazo ndani yako, nguvu zilizomfufua Yesu ni hii: *“Imani uliyonayo kwa Mungu, katika Yesu Kristo, na katika neno lake – inapata uhai na inakuwa na uwezo wa kuzaa”!* Hii ni kwa sababu biblia inasema “tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na Imani yenu ni bure” (1 Wakorintho 15:14). Hebu oanisha maneno ya mstari huu na maneno ya mistari hii: “Imani isipokuwa na matendo, imekufa nafsini mwake” (Yakobo 2:17). “Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?” (Yakobo 2:20). “Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa” (Yakobo 2:26). Imani uliyonayo kwa Mungu katika Kristo, na katika neno lake inatakiwa iwe hai! Imani yako hiyo isipokuwa hai ndani yako ni bure…yaani inakuwa haina faida kwako, wala msaada wowote kwako! Ina maana ni imani usiy...